YANGA WACHEKELEA SANGA KUJIUZULU

Kufuatia Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kuachia ngazi jana, baadhi ya wadau na wachama wa Yanga wengi wamepongeza uamuzi huo.


Wanachama hao wamekubaliana na maamuzi ya Sanga huku wengi wakieleza ni sahihi kwake kufanya hivyo kutokana na mwenendo mzima wa klabu ulivyo sasa.


Mbali na mwenendo wa klabu, wachama hao wamesema Sanga alikuwa amechelewa wakieleza alipaswa kufanya hivyo mapema ili kuwapa nafasi wengine.


Wengi wao wamefunguka na kueleza Sanga alikuwa haiendeshi Yanga kwa ueledi na kupelekea kuleta kutokuelewana baina yake na viongozi wengine haswa wa kamati ya utendaji waliojiuzulu akiwemo Khalfan Hamis.


Kitendo cha Sanga kuachia ngazi kimewakonga nyonyo wachama hao pamoja na baadhi ya mashabiki kwa maamuzi yake na sasa itabidi ikiwezekana uchaguzi ufanyike ili mbadala wa Mwenyekiti apatikane.


Sanga ameeleza sababu mojawapo iliyompelekea kuachia ngazi ni kushutumiwa na baadhi ya watu akisema walipanga kwenda kuvamia kwake wakiwa na mapanga jambo ambalo ameona linaweza kuhatarisha maisha yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527