WEMA SEPETU AHUKUMIWA JELA MWAKA MMOJA KWA KUTUMIA BANGI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 20, 2018

WEMA SEPETU AHUKUMIWA JELA MWAKA MMOJA KWA KUTUMIA BANGI

  Malunde       Friday, July 20, 2018
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya aina ya Bangi nyumbani kwake.


Akisomewa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018 katika Makahama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Wema Sepetu ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumikia adhabu hiyo.


Katika hukumu nyingine wafanyakazi wawili wa ndani wa msanii huyo ambao nao walitajwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kukutwa bila hatia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post