HIZI NDIYO KLABU ZILIZOCHANGIA MAGOLI MENGI KOMBE LA DUNIA


Mfungaji aliyeongoza kufunga magoli mengi kwenye kombe la dunia Harry Kane akiwa anatokea katika klabu ya Tottenham Hortspur na timu ya England.

Klabu ya PSG ya Ufaransa naTottenham Hortspur ya nchini Uingereza zimeongoza katika listi ya vilabu vilivyochangia mabao mengi katika michuano ya kombe la Dunia iliyomalizika hivi karibuni nchini Urusi.


PSG imeongoza ikiwa imechangia jumla ya magoli 12, magoli manne kati ya hayo yakifungwa na Kylian Mbappe na mengine yakifungwa na Edinson Cavani (3), Neymar (2), Thomas Meunier, Angel Di Maria na Thiago Silva.

Spurs nayo imelingana na PSG kwa kutoa wachezaji waliofunga jumla ya magoli 12 katika michuano hiyo huku mchezaji, Harry Kane akifunga magoli 6 peke yake na mengine yakifungwa na, Heung Min Son (2), Christian Eriksen (1), Dele Alli (1), Kieran Trippier (1) na Jan Vertonghen.

Klabu ya Barcelona imechangia magoli 11 na wafungaji wakiwa ni Yerry Mina (3), Phillipe Coutinho (2), Luis Suarez (2), Lionel Messi (1), Samuel Umtiti, Ivan Rakitic na Paulinho ambaye amejiunga na klabu ya Ghuangzhou Evergrande kwa mkopo baada ya kombe la Dunia kumalizika .

Real Madrid imekamata nafasi ya tatu ikiwa imetoa wachezaji ambao wamefunga jumla ya magoli 10 kwenye michuano hiyo, wafungaji ni Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na Juventus wiki chache zilizopita akifunga magoli manne, Luka Modric (2), Nacho, Isco, Raphael Varane na Toni Kroos.

Klabu zingine zilizochangia magoli mengi ni Atletico Madrid na Manchezter United zilizochangia magoli 8, Villa Real na Manchezter City zikichangia magoli 5, Liverpool, Chelsea, Juventus na CSKA Moscow zikichangia magoli manne.

Michuano hiyo imemalizika kwa Ufaransa kuibuka bingwa kwa mara ya pili katika historia yake, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1998 huku kocha Didier Deschamps akiweka rekodi ya kuwa kocha wa tatu kuchukua kombe hilo akiwa mchezaji na kocha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527