Wednesday, July 11, 2018

WAVULANA WOTE 12 NA KOCHA WAO WALIONASA PANGONI WAOKOLEWA

  Malunde       Wednesday, July 11, 2018
Wavulana 12 wa timu ya soka Thailand na kocha wao wameokolewa salama kutoka ndani ya pango walimokuwa wamekwama kwa siku 17 kaskazini mwa Thailand.

Mkasa huu uliwagusa wengi duniani, waliofuatilia kwa makini jitihada za kuwakoa.

Kikosi cha wanajeshi wa maji nchini kilichosimamia operesheni hiyo ya uokozi wanasema wavulana hao a kocha wao wameokolewa salama na kukamilisha operesheni iliyokuwa ngumu na ya hatari.

Kundi hilo la vijana wacheza soka walikwama ndani ya pango tangu Juni 23 baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha pango kufurika maji.

Awali duru iliyokuwa ndani ya operesheni hiyo ya uokozi imeiambia BBC kwamba watu watatu wametolewa kutoka kwenye pango hilo leo.

Operesheni hiyo iliendelea leo wakati wavulana wanne, kocha wao na daktari na wanajeshi watatu wa maji wakiwa ndani ya pango hilo.Ambulensi zilionekana zikiondoka kutoka eneo la pango hilo la Tham Luang

Waziri mkuu wa Thailand awali alithibitisha ripoti kwamba vijana hawa walipewa dawa ili kuwasaidia wasishikwe na wasiwasi wakati wakiokolewa.

Hapo jana Wapigaji mbizi kaskazini mwa Thailand wamewaokoa wavulana wanne zaidi kutoka pango lililofurika maji.

Hii inaashiria kuwa kwa jumla, wavulana 8 wameokolewa salama huku watu watano wakiwa bado wamesalia ndani ya pango.

Wavulana wengine 4 waliokolewa salama kutoka pangoni siku ya Jumapili.Mamilioni ya lita za maji yametolewa ili kurahisisha shughuli ya uokozi

Wavulana hao wameondolewa kwa njia gani?

Kundi la wataalamu wa kupiga mbizi 90 kutoka Thailand na 50 kutoka nchi za kigeni wamekuwa wakifanya kazi kwenye pango hilo.

Wamekuwa wakiwaelekeza wavulana hao kwenye giza na maeneo yaliyofurika maji kwenda mlango wa pango.

Kufika mahala wavulana hao wapo na tena kufanya safari ya kurudi ni kazi ngumu hata kwa wapiga mbizi wenye ujuzi.

Shughuli hiyo imejumuisha kutembea, kupanda na kupiga mbizi wakifuata kamba ambazo tayari zipo pangoni.

Akiwa amebeba vifaa vya hewa kila mvulana huandamana na wapiga mbizi wawili ambao pia hubeba hewa yake ya kupumua.

M
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post