WAFANYABIASHARA KAKONKO NA CANKUZO BURUNDI KUDUMISHA UMOJA WAO ZAIDI

Wafanya biashara wilayani Kakonko na  mkoa wa Cankuzo nchini Burundi wametakiwa kudumisha umoja wao kwa kubadilishana fursa na bidhaa kwa kutumia masoko ya ujirani mwema yaliyojengwa mipakani.

Akizungumza juzi katika kikao cha Biashara cha ujirani mwema kilichofanyikawilayani Kakonko kikiwakutanisha wafanyabiashara wa wilaya ya Kakonko na mkoa wa Cankuzo kutoka Burundi na viongozi wengine wa mkoa  huo, Mkuu wa wilaya ya Kakonko  Kanali Hosea Ndagala aliwataka wafanyabiashara kutoka Burundi kuwekeza Kakonko kwa kuwa serikali imeboresha miundombinu ya dbarabara, umeme na ujenzi wa masoko ya Kimataifa ili kuvutia wawekezaji.

Alisema mwingiliano huo utaendelea kudumisha umoja wa nchi za Afrika Mashariki  ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi wa wafanya biashara wa Burundi na Tanzania kwa kutumia fursa zilizopo pande mbili na kubadilishana uzoefu wa biashara kwa kuwa viongozi wanaendelea kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo yote ya masoko na kuhakikisha masoko yote yanayojengwa yanakuwa na vituo vya polisi na huduma zote.

Mkuu huyo alisema zipo fursa nyingi za kibiashara na kilimo pamoja na ufugaji na nishati  katika wilaya ya Kakonko na kuwaomba wafanya biashara wa Burundi kuja kuwekeza vituo vya mafuta maeneo yapo na zipo fursa za viwanda  fursa katika wilaya ni nyingi kwa wafanya biashara na fursa ya masoko ipo serikali inatarajia kujenga soko kuu la ujirani mwema katika Kijiji cha Muhange ambapo kutakuwa na huduma zote za msingi.

Naye mkuu wa mkoa wa Cankuzo Nchini Burundi Njiji Dezire alisema kwa Burundi wengi wao wafanya biashara wanategemea bidhaa kutoka Tanzania kwa mkoa wao ni wazarishaji wa maparachichi na kuomba umoja huo uendelee kwa kuwa unaendelea kujenga uchumi mzuri wa nchi zote mbili na kujenga ushirikiano mzuri.

Alisema suala la ulinzi na usalama wanaendelea kulidumisha kwa kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu na kuhakikisha mipaka inakuwa salama na wananchi wa nchi zote mbili wanaingia na kutoka kwa kufuata utaratibu ilikuepusha usumbufu na kuomba serikali ya Tanzania kukamilisha madaraja yaliyopo katika njia ambazo zinatumika ili wananchi wasiwe wanaingia kwa kutumia njia za panya.

Mwenyekiti wa Chama cha biashara wakulima na wafugaji wilayani Kakonko alisema mwaliko wa wafanyabiashara wa Kakonko waliomualika na wageni wote kutoka Burundi mkoa wa Cankuzo kudumisha umoja wa Afrika mashariki na ni mwendelezo wa ziara zinazofanyika kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi kubadilishana uzoefu wa biashara na kubadilishana fursa hiyo ni  hatua nzuri ya kujiletea maendeleo kwa wananchi wa nchi mbili

Soko litagharimu milioni  mia nne na ni soko la kisasa.

Suala la ulinzi na usalama bila ulinzi na usalama hakuna kinachoweza kufanyika, Kakonko ulinzi umeimarika na matukio ya utekaji kwa sasa hayapo.

Hata hivyo, kumezuka wizi wa pikipiki jirani na wilaya ya Kakonko maeneo ya Kahama wezi wanateka pikipiki pamoja na kuuwa pikipiki zinavushwa kupitia Muhange kuingia Kisagara na kuomba kukamata pikipiki zote ambazo hazina kibali. 

Mwingiliano ni mkubwa wananchi kuingia kwenda kulima nchi nyingine .

Mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara, Kilimo na Ufugaji Tito Joseph alisema wamekuwa na ushirikiano mzuri na wafanya biashara kwa kuwauzia bidhaa mbali mbali hasa magodoro na wao wamekuwa wakiende kwenye vikao vya kubadilishana uzoefu wa biashara kwa kwenda kufanya vikao kama hivyo kwa nchi ya Burundi.

Alisema umoja huo watauendeleza na kuwaomba wafanya biashara kuendelea kushirikiana na kuwasilisha changamoto watakazo ziona katika wilaya hiyo   kuzifanyia kazi na kuhakikisha biashara wanazozifanya zinakuwa na tija na zinawazalishia ipasavyo.

Kwa upande wao baadhi ya wafanya biashara wa Cankuzo akiwemo Ndakirwe  Emeline alisema wao kama wafanyabiashara wamekuwa wakija Tanzania kufanya biashara changamoto ambayo wamekuwa wakikutana nayo ni baadhi ya wanajeshi walioko mipakani kuwasumbua wanapotaka kuingia nchini hata wakiwa na vibali.

Alisema wapo baadhi ya wafanya biashara wamekuwa wakinyang'anywa fedha zao wanaokuja kufanya biashara na kuomba Viongozi kutatua changamoto hiyo kwa kuendelea kudumisha  ulinzi na usalama kwa wafanya biashara wa Burundi na Tanzania.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Cankuzo nchini Burundi Njiji Dezire  akizungumza na viongozi na wafanya biashara wa wilaya ya Kakonko  na wa mkoa wa Cankuzo.Picha na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Baadhi ya wafanya biashara wa wilaya ya Kakonko  na mkoa wa  Cankuzo nchini Burundi  wakibadilishana uzoefu kikao cha ujirani mwema Kakonko.
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala  akizungumza na wafanya biashara wa Kakonko na mkoa wa Cankuzo nchini Burundi  wilayani Kakonko mkoani Kigoma


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527