SHULE YA SEKONDARI MAGUFULI YAONGOZA KIMKOA MATOKEO KIDATO CHA SITA

Shule ya Sekondari Magufuli iliyopo wilayani Chato, Geita imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya shule 10 zilizopo mkoani Geita.


Shule hiyo pia imeshika nafasi ya 18 kitaifa ambapo watahiniwa wote 82 wamefaulu.


Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo Julai 13, wanafunzi 40 kati yao wamepata daraja la kwanza 40 wengine daraja la pili na wawili daraja la tatu.


Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joel Hari amesema shule hiyo imeonyesha juhudi kwani mwaka jana ilishika nafasi ya pili kimkoa na kitaifa ilishika nafasi ya 28.


Mbali na shule ya Magufuli pia shule ya wasichana ya Jikomboe ya wilayani humo imeshika nafasi ya nne kimkoa huku shule ya Chato ikishika nafasi ya saba kimkoa.


Hari amewapongeza walimu na idara ya elimu sekondari katika wilaya hiyo kwa jitihada kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu.


Wilaya ya Chato ina shule 27 za sekondari ambapo kati ya hizo shule tatu ni za kidato cha tano na sita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527