Wednesday, July 18, 2018

RATIBA MPYA YA LIGI KUU BARA MSIMU WA 2018/2019 IMETOKA

  Malunde       Wednesday, July 18, 2018
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limetangaza ratiba mpya ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 itakayoanza Agosti 22 2018.


Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema ligi hiyo itahusisha jumla ya mechi 380 kutoka 240 ambazo zilikuwa zilichezwa msimu uliopita kutokana na ongezeko la timu.


Wambura ameeleza katika msimu wa 2017/18 ligi ilihusisha jumla ya timu 16 pekee lakini kuelekea msimu ujao kutakuwa na idadi ya timu 20 ambazo zimefanya kuwe na ongezeko la idadi ya mechi.


Yanga itaanzia ugenini huko Morogoro Agosti 23 kucheza na timu ya Mtibwa Sugar huku Azam FC wakianza nyumbani kukipiga na Mbeya City. 

Ratiba hiyo inaonesha pambano la watani wa jadi litapigwa Septemba 20 kwenye uwanja wa taifa na Simba watakuwa wenyeji wa Yanga. 

Kwa upande wa timu zilizopanda ligi kuu msimu huu Alliance watacheza na Mbao FC, Biashara United wakianza na Singida United. JKT Tanzania watakipiga na KMC, African Lyon watacheza na Stand United huku Coastal Union wakicheza na Lipuli FC.

Aidha Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amesema mechi ya Ngao ya Jamii kati ya bingwa Simba na bingwa wa kombe la shirikisho Mtibwa Sugar itapigwa Agosti 18 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Msimu huu utashirikisha jumla ya timu 20 kutoka 16 zilizoshiriki msimu uliopita. Timu tatu zitakazoshika nafasi za chini moja itashuka moja kwa moja huku mbili zikicheza mechi na washindi wa pili na tatu wa ligi daraja la kwanza na wakifungwa wanashuka ila wakishinda wanabaki ligi kuu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post