RAIS MAGUFULI : MTAPATA MAENEO YA KUPIGIA PICHA NA KUFUNGIA NDOA


Rais Dkt. John Magufuli

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa daraja jipya la Salenda, litakuwa ni ukurasa mpya wa kutengeneza mandhari ya jiji la Dar es salaam kutokana na muonekane wake litapomalizika kujengwa.

Rais Magufuli amesema hayo wakati wa zoezi la utiaji saini kati ya wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo kutoka nchini Korea, ambapo amesema kuwa anatarajia ujenzi huo utakuwa ni wa muda mfupi kwakuwa watendaji wapo wa kutosha nchini.

“Ntashangaa sana kama huyu 'Contractor' wa kutoka nchi kubwa kama Korea kama atahangaika miezi yote 36 kuitumia katika ujenzi wa daraja hili , wakati kama ni fedha zipo na kama ni vibarua Tanzania wamejaa tele”, amesema Rais Maguli.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa, “Nina uhakika sasa watani zangu wazaramo watakuwa na maeneo mengi ya kupiga picha na kufungia ndoa”.

Zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Selander Jijini Dar es Salaam, limeshuhudiwa pia na Waziri Mkuu wa Korea, Lee Nak-yon ambaye yupo katika ziara ya kikazi nchini.

Daraja hilo litajengwa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu, ambapo litaunganisha barabara ya Barack Obama na eneo la Coco Beach katika makutano ya barabara za Kenyatta na Toure.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527