RAIS MAGUFULI ATEUA WALIOHAMA UPINZANI KUWA WAKUU WA WILAYA



Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wa wilaya na makatibu tawala nchini huku akiwateua wanasiasa watatu waliowahi kuwa vyama vya upinzani katika nafasi hizo.


Akitangaza mabadiliko hayo leo Julai 28, Rais Magufuli amemteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.


Kafulila aliwahi kuwa mbunge wa NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.


Pia amemteua Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Machali aliwahi mbunge wa Kasulu Mjini, (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo na baadaye CCM.


Kadhalika Rais Magufuli amemteua Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Katambi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527