Wednesday, July 4, 2018

Picha : DC SHINYANGA AZINDUA CHANJO YA KINGA NA TIBA YA MAGONJWA YA MINYOO NA KICHOCHO

  Malunde       Wednesday, July 4, 2018
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amezindua zoezi la Chanjo ya kinga na tiba ya magonjwa ya minyoo na kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi mjini Shinyanga.

Matiro amezindua chanjo hiyo leo  Jumatatno Julai 4,2018 katika shule ya Msingi Town manispaa ya Shinyanga  kwa kuwapatia vidonge vya kinga ya magonjwa hayo wanafunzi nane  ambapo katika shule hiyo jumla ya wanafunzi 1,046 wamepewa chanjo hiyo. 

Alisema zoezi hilo litaendeshwa kwa wanafunzi wote kuanzia umri wa miaka mitano hadi 14, ambapo jumla ya wanafunzi 41,465 wa mjini Shinyanga ndio watapata chanjo ya kinga ya magonjwa hayo ya minyoo na kichocho ili kuwafanya wawe na afya njema na hatimaye kufaulu vizuri masomo yao. 

“Chanjo hii dhidi ya magonjwa haya ya minyoo na kichocho ni salama kabisa, hivyo naomba wanafunzi wote mshiriki zoezi hili ili kulinda afya zenu, na kuwafanya mjikite zaidi kwenye masomo,”alisema Matiro. 

“Naomba pia muachane na tabia ya kuogelea kwenye madimbwi, kula bila ya kunawa mikono,kujisaidia hovyo pamoja na kunywa maji ambayo hayajachemswa, mkifanya hivyo kamwe magonjwa ya minyoo na kichocho hamuwezi kuyapata,”aliongeza. 

Naye Ofisa Elimu wa Sayansi kimu na afya manispaa ya Shinyanga Beatrice Bonea ,alisema zoezi hilo litaendeshwa kwa shule zote za msingi manispaa hiyo, kwa kupatiwa chanjo hiyo ya kinga na tiba kwa magonjwa ya minyoo na kichocho. 

Nao baadhi ya wanafunzi waliopata kinga ya chanjo ya magonjwa hayo akiwemo Lazina Hamza darasa la tano, aliipongeza serikali kwa kuwapatia kinga hiyo ambayo itawafanya kuwa na afya njema, ikiwa idadi kubwa ya wanafunzi hua wanatabia ya kula vitu hovyo bila ya kunawa mikono.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho na kuwataka wanafunzi kuzingatia elimu waliyopata ya kutokunywa maji ambayo hayajachemshwa, kutojisaidia hovyo,kutokula bila ya kunawa mikono pamoja na kutoogelea kwenye madimbwi ya maji yaliyotuama.- Picha na Marco Maduhu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiuliza maswali wanafunzi wa shule ya Msingi Town juu ya umuhimu wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichochona kumjibu kuwa itasaidia kuepukana na magojwa hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kuuliza maswali wanafunzi juu ya umuhimu wa kupewa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwataka Wanafunzi hao kujitokeza wote kupewa chanjo hiyo ambayo itawasaidia kuwa na afya njema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akinawa mikono kabla ya kuzindua zoezi chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho katika shule ya Msingi Town iliyopo mjini Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpatia Mwanafunzi kidonge cha kinga hiyo ya magonjwa ya minyoo na kichocho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpatia kidonge cha kinga ya magonjwa ya minyoo na kichocho Mwanafunzi Lazina Hamza wa darasa la tano katika shule ya msingi Town.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Town wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho
Wadau wa afya wakiwa kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Wadau wa afya wakiwa kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro mkono wa Kushoto akiwa na Ofisa Elimu Sayansikimu na Afya manispaa ya Shinyanga Beatrice Bonea wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza muziki wa Diamond (Kwangwaru) na wanafunzi wa shule hiyo ya Msingi Town mara baada ya kumaliza kuzindua zoezi hilo lachanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Muziki ukiwa umekolea.
Burudani ikiendelea kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasili katika shule ya msingi Town Tayari kwa uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Town manispaa ya Shinyanga Said Juma akiipongeza serikali kwa kutoa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho kwa Wanafunzi.
Wacheza Ngoma wa Kikundi cha Wagoyangi wakitoa Burudani kwenye uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Wapiga ngoma wa kikundi cha Wagoyangi wakitoa burudani.
Ofisa Elimu wa Sayansikimu na Afya manispaa ya Shinyanga Beatrice Bonea akizungumza kwenye zoezi hilo kuwa litaendeshwa leo kwa shule zote za msingi manispaa hiyo, kwa kupatiwa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho
Wadau wa afya wakiwa kweye uzinduzi huo wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho manispaa ya Shinyanga.
Kikundi cha Ngoma Wagoyangi wakiendelea kutoa burudani kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Burudani ikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiagana na Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Town Said Juma mara baada ya kumaliza kuzindua chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiagana na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kuzindua zoezi hilo la uzinduzi wa chanjo ya kinga na tiba ya minyoo na kichocho, Manispaa ya Shinyanga.
Picha na Marco Maduhu
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post