NAIBU WAZIRI WA NISHATI AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI REAIII MOROGORO


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA Awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Julai 9, 2018. Mhe. Naibu Waziri pia alitumia fursa hiyo kusikiliza kero za wananchi kuhusu upatikanaji umeme kwenye vijiji vyao. K-VIS BLOG, MOROGORO

******

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, amezindua mradi wa usambazaji umeme vijini REA awamu ya tatu (REAIII), ambapo jumla ya vijiji 180 vya Mkoa wa Morogoro vitanufaika.

Naibu Waziri alifanya uzinduzi huo kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani humo Jumatatu Julai 9, 2018 kwa kukata utepe na kuwasha swichi ya umeme na hivyo kuibua shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa wananchi waliojawa na furaha.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, alisema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inayo dhamira ya kweli ya kuhakikisha ahadi zote
ilizotoa kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wote wa Tanzania mijini na vijijini inatekelezwa kwa kasi.

“Tayari umeme umefika sasa utumieni kika milifu kujiletea maendeleo yenu na taifa kwa ujumla”,lisema Mhe. Naibu
Waziri.

Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni nafuu sana kiasi cha shilingi Elfu Ishirini na Saba tu (27,000).
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi kuhusiana na mradi wa umeme vijijini (REA) REA Awamu ya Tatu
(REAIII) mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro. 
Wananchi wakimsikilzia Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakayti akihutubia
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa 
Diwani wa kata ya Kimamba A, Upendo Mpoto akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu wakati akisikiliza kero zinazohusiana na mradi wa umeme vijijijini.
Diwani wa Kata ya Kimamba akizungumza kwenye mkutano huo. 
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (Mwenye Kilemba chekundu kichwani) akimsikiliza Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Bw. Stephen Lukobe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maful. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Maganga.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu kulia akizungumza jambo na Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa, Stephen Lukobe katika ofisi ya kijiji cha Madudu wakati wa ziara ya naibu waziri huyo ya kutembelea vijiji vitavyonufaika na mradi wa umeme wa REA Awamu ya tatu (REAIII), mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro Julai 9, 2018
Mkazi wa kijiji cha Mandera, Wilayani Kilosa, akizungumza mbele ya Naibu Waziri

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527