KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MITAMBO YA MKONGO WA TAIFA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (Wa tatu kulia), akiwaelekeza jambo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea mitambo ya Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa unaoendeshwa na TTCL Corporation.
Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (wa kwanza kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea sehemu ya mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano jijini Dar es Salaam inaoendeshwa na TTCL Corporation. 
Mtaalamu wa mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea mitambo ya Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa unaoendeshwa na TTCL Corporation.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge.
Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (katikati) akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kutembelea mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano jijini Dar es Salaam inaoendeshwa na TTCL Corporation.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527