MWANZA WAZINDUA KAMPENI YA 'AFYA YANGU, FURAHA YANGU'


Mkoa wa Mwanza umezindua kampeni ya ‘Afya Yangu Furaha Yangu’ inayolenga kuhamasisha upimaji virusi vya Ukimwi.

Akizungumza leo Julai 21,2018 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Mwanza Dkt. Pius Masele amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka asilimia 4.2, mwaka 2011.

Kwa mujibu Dk Masele amesema ongezeko hilo linaufanya mkoa huo kuwa wanne ukitanguliwa na Njombe,Iringa na Mbeya.

Dk Masele ameeleza mikakati ya kupunguza maambukizi hayo ni kuzifikia 90 tatu, ifikapo kwama 2030.

Amesema 90, 90, 90 zinamaanisha kupunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 90 ifikapo 2030, asilimia 90 ya wananchi kupima ifikapo mwaka huo na asilimia 90 kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi.

Na Ngollo John, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527