MSIBA WA PATRICK WAMUIBUA LULU


Baada ya kimya cha muda mrefu, msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama Lulu leo ameibuka na kuweka picha ya mshumaa kwenye mtandao wake wa Instagram.

Picha hiyo ameiweka leo Julai 4,2018 akiomboleza kifo cha mtoto wa rafiki yake, Muna Love.

Mtoto huyo, Patrick alifariki dunia Nairobi, Kenya jana usiku wa Julai 3,2018 akipata matibabu.

Lulu hajaonekana hadharani tangu alipotoka jela Mei mwaka huu.
Na Nasra Abdallah, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.