Friday, July 6, 2018

MKE AMUACHA MUMEWE KISA NI HANDSOME....ANAPATA TABU SANA KWENYE NDOA

  Malunde       Friday, July 6, 2018

Mwanamke mmoja Raia wa Saudi Arabia amemuacha Mume wake sababu ikiwa ni mzuri sana (handsome).

Mwanamke huyo ambaye jina lake halijaanikwa hadharani amedumu kwenye ndoa na Mumewe huyo kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo amesema kuwa alikuwa akiishi kwa wasiwasi kutokana na kuhofia kunyang’anywa na Wanawake wengine.

Inadaiwa kuwa kutokana na uzuri wa Mumewe, Mwanamke huyo amekuwa na wivu sana na kushindwa kumuamini kabisa Mumewe akihisi kuwa huenda atakuwa anachepuka na Wanawake wengine ambao watakuwa wanachanganyikiwa na uzuri wake.

Aidha Mwanamke huyo amesema kuwa ameamua kufikia maamuzi hayo ili aishi kwa amani maana kuishi na Mume wake huyo ambaye ni daktari kulikuwa kunampa msongo wa mawazo na kumfanya awe na wasiwasi kila wakati.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post