MEYA AWATAKA ASKARI WA KIKE KUVAA NGUO FUPI KUONGEZA MVUTO


Mabinti wa vyuo waliojiliwa na Jeshi la Polisi nchini Lebanon.

Meya wa mji wa Broummana nchini Lebanon Pierre Achkar amewaajili warembo wa vyuo vikuu katika kitengo cha maafisa usalama barabarani huku akiwapa masharti ya kuzingatia.

Pierre ametoa nafasi hiyo kwa mabinti wa vyuo vikuu kuajiliwa ili kufanya kazi na maafisa usalama barabarani huku akiwataka kuvaa nguo fupi kwa kile alichodai kuwa ni sehemu ya kuvutia vyombo vya habari, ndani na nje ya nchi.

"Sababu kubwa ya kuajili mabinti hawa ni kuongeza mvuto katika maeneo yetu ya mji na kuvutia vyombo vya habari ambapo tutapata namba kubwa ya watalii na kukuza uchumi wa nchi yetu”,amesema Pierre.

Hili ni agizo la pili kutoka kwa Pierre baada ya siku chache zilizopita kutoa agizo kwa walimu wa mazoezi ya viungo kufundisha mabinti pembezoni mwa barabara mjini Broummana ili kuwavutia watalii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527