Saturday, July 14, 2018

SHULE YA WASICHANA ST.MARY'S MAZINDE JUU YANG'AA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018

  Malunde       Saturday, July 14, 2018

Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga imeendelea kuubeba mkoa wa Tanga baada ya kushika nafasi ya nane na kuwa kwenye 10 bora ya shule zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

Pamoja na kushika nafasi hiyo, pia wanafunzi wake sita wapo kwenye 10 bora za kitaifa, ambapo wawili wapo 10 bora kitaifa na wanne wameingia 10 bora ya wasichana kitaifa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Julai 13, 2018 ofisini kwake, Mkuu wa Shule hiyo Mtawa Evetha Kilamba, alisema mafanikio hayo ni makubwa kwenye shule yao, kwani pamoja na wanafunzi hao wanne kuwa kwenye 10 bora, hata wengine waliobaki wamefanya vizuri.

"Wanafunzi wetu wawili wameingia 10 bora kitaifa, ambapo Emmy S. Shemdangiwa (PCB) ameshika nafasi ya tisa na Vanessa Lodrick Show (PCB) ameshika nafasi ya kumi. Kwa upande wa wasichana 10 bora kitaifa, Emmy S. Shemdangiwa (PCB) ameshika nafasi ya tatu, Vanessa Lodrick Show (PCB) akakamata nafasi ya nne, Diana Maziku Chenya (PCM) nafasi ya saba na Christina John Mjema (PCM) nafasi ya nane. Lakini kwenye masomo ya sanaa na lugha, Tumaini Irene Mboya ameshika nafasi ya nane (8) kitaifa na kwa wasichana ameshika nafasi ya tatu (3), huku Lina J. Meena akishika nafasi ya tano (5) kwenye masomo ya lugha kitaifa.


"Lakini pia tumefanikiwa kushika nafasi ya nane kitaifa kati ya shule 543 Tanzania na nafasi ya kwanza kimkoa katika Mkoa wa Tanga kati ya shule 25. Pia kati ya wanafunzi wetu 189 waliofanya mtihani huo, 133 wamepata daraja la kwanza, 52 daraja la pili na daraja la tatu ni wanne, shule yetu haina daraja la nne wala sifuri. Kiwango cha wanafunzi kupata daraja la kwanza ni kikubwa kuliko shule yeyote nchini kwa mwaka huu" ,alisema Mtawa Kilamba.

Kilamba amewashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha wanafunzi hao kufanya vizuri wakiwemo walimu wa shule hiyo, uongozi wa shule ikiwemo Bodi ya Shule, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Mhashamu Anthony Banzi, Afisa Elimu Wilaya ya Lushoto na wazazi kwa kuweza kulipa ada kwa wakati.

"Kwanza namshukuru Mungu kwa mafanikio haya. Najivunia shule yetu kuubeba Mkoa wa Tanga kwa kufanya vizuri. Mafanikio haya yametokana na ushirikiano uliopo kati ya wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Masista wa Usambara Mtawa Gaspara Kashamba" ,alisema Mtawa Kilamba.

                        Imeandikwa na Yusuph Mussa, Lushoto
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Emmy S. Shemdangiwa (PCB) ambaye amekuwa wa tisa kwenye wanafunzi 10 bora kitaifa na kushika nafasi ya tatu kwa wasichana 10 bora kitaifa masomo ya sayansi mtihani wa kidato cha sita 2018.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Vanessa Lodrick Show (PCB) ambaye amekuwa wa 10 kwenye wanafunzi 10 bora kitaifa na kushika nafasi ya 4 kwa wasichana 10 bora kitaifa masomo ya sayansi mtihani wa kidato cha sita 2018.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Tumaini-Irene Mboya ambaye ameshika nafasi ya tatu kwa wasichana 10 bora kitaifa kwenye masomo ya sanaa na lugha mtihani wa kidato cha sita 2018.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Lina Joram Meena ameshika nafasi ya tano kwenye wanafunzi 10 bora kitaifa wa masomo ya sanaa na lugha katika mtihani wa kidato cha sita 2018.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Christina John Mjema ambaye amekuwa wa 8 kwenye wasichana 10 bora kitaifa kwenye masomo ya sayansi (PCM) mtihani wa kidato cha sita 2018.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Diana Maziku Chenya (PCM) ambaye amekuwa wa 7 kwenye wasichana 10 bora kitaifa kwenye masomo ya sayansi (PCM) mtihani wa kidato cha sita 2018.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana St. Mary's Mazinde Juu iliyopo wilayani Lushoto mkoani Tanga Evetha Kilamba akiwa ofisini kwake eneo la Magamba.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu iliyopo wilayani Lushoto mkoani Tanga wakiwa nje ya jengo la utawala. (Picha kwa hisani ya Yusuph Mussa).
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post