SHINYANGA WAMLILIA DC JOSEPHINE MATIRO .....JASINTA VENANT AVAA KIATU CHAKE

Josephine Matiro

Leo Jumamosi Julai 28,2018 Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika nafasi mbalimbali za kiuongozi wakiwemo wakuu wa wilaya,mikoa na makatibu tawala.


Saa chache baada ya kuwepo kwa taarifa za mabadiliko hayo,wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wamekuwa na mitazamo mbalimbali kuhusu wateule wapya lakini pia viongozi walioondolewa katika nafasi walizokuwa wanazitumikia.

Katika Mabadiliko hayo,miongoni mwa walioguswa ni Bi Josephine Matiro aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga hadi leo Julai 28 ambaye nafasi yake imechukuliwa na Bi Jasinta Venant ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo ya Shinyanga.

Kuachwa kwa Bi. Josephine Matiro kumezua gumzo mitaani na hata kwenye mitandao ya kijamii watu wengi wamekuwa wakiishia kusema ‘Ama kweli vizuri havidumu’.

Unaweza kusema,mabadiliko yaliyofanywa na rais Magufuli yameleta kilio kwa baadhi ya wakazi wa Shinyanga ambao wanasema,Matiro alikuwa kiongozi mchapakazi aliyependa wananchi bila kujali hali zao.

Malunde1 blog imepata baadhi ya maoni ya wananchi ....soma hapa chini

➤Maumivu niliyoyapata kuhusu Matiro,daah sijawahi kuumia hivyo…..Alikuwa DC mahiri haijawahi tokea kwa Shinyanga….Alipenda kusimamia kwenye ukwel haki na usawa.

Alikuwa ni mama mchapakazi, mwenye hofu na Mungu!!!


Hatuna jinsi. MUNGU atie nguvu dada tulimpenda, tulimzoea alitusaidia. Basi tu Mungu atampa mlango wa kutokea. Amen.

Huyu mama nilimpenda sana japo sipo huko ila nilikuwa naona anavyopambana bega kwa bega

Kiukweli... Alikuwa mchapakazi sana... Vizuri havidumu...Ntammiss pia

Dah Matiro wetuuuu ukweli chama hakiishi

Yaani mkuu Josephina matiro  nimesikitika Sana nikiangalia alivyo kuwa Duuu Sina usemi tusubirie mengine haya yameshapita 😞

Kasema watapangiwa kazi nyingine subirini uteuzi atakao teuliwa

Mi binafsi nimeumia kwakweli jamani

Vizuri ndugu huwa havidumu sijui kwa nini? Tumwachie MUNGU.
Wachapakazi huwa hawakai sijui ni kitu gani,tulipata Matiro na Malecela lakini ndio hivyo!!🙏🙏🙏Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kila jambo

Kweli wazuri hawadumu ingawa uongozi ni kupokezana kijiti mkuu wetu wa wilaya shinyanga ameondolewa wakati tulikuwa tukimhitaji alikuwa mtu wa watu mpambanaji na msimamia ukweli ila tunaamini mungu atamfungulia mlango mwingine

But... I have faith...God has prepared something greater for her...

BOFYA <<HAPA>> KUANGALIA MATUKIO YALIYOFANYWA NA DC JOSEPHINE MATIRO SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527