Tuesday, July 10, 2018

WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA - MARYNESS NA ANISIA WASAFIRISHWA

  Malunde       Tuesday, July 10, 2018

Mapacha walioungana

Watoto mapacha walioungana Maryness na Anisia Beatusi, wamepelekwa nchini Saudia Arabia kwa matibabu baada ya kupata ufadhili kutokana na uhusianao mzuri baina ya serikali ya Tanzania na nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Saudia Arabia nchini Mohammed El Malik amesema mfalme wa Saudia amewafadhili watoto hao baada ya ombi lilitolewa na serikali ya Tanzania.

Akizungumzia upasuaji huo daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Petronila Ingiloi amesema kuwa wamepata ugumu hasa kwenye matokeo ya mwisho baada ya kufanikisha upasuaji wa watoto hao.

Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji watoto, Zaituni Buhari ambaye anaye safiri na watoto hao amesema uchunguzi wa awali utafanywa kwa umakini ili kuweza kufanikisha upasuaji salama kwa watoto hao.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post