MAMA AKUTWA AKIISHI NA MAITI YA MWANAE ALIYEFARIKI MWAKA 2017

 Mama mmoja nchini Marekani amewashangaza wengi baada ya kukutwa akiwa anaishi na maiti ya Mwanae aliyefariki Novemba 2017.

Majirani wa Mama huyo anayeishi katika mji wa Detroit wamesema kuwa Mama huyo hakuripoti kifo cha Mwanae kwa Polisi bali aliendelea kuishi na maiti hiyo pasipo Watu kujua.

Inaelezwa kuwa Mtoto huyo ambaye kwa sasa angekuwa na miaka 47 alikuwa na matatizo ya kiafya ingawa kifo chake bado kinafanyiwa uchunguzi na jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa sheria za mji wa Detroit ambapo Mama huyo anaishi zinasema kuwa ni kinyume na sheria kwa Mtu wa mji huo kutoripoti kifo kwa Polisi na adhabu yake inaweza kuwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.