Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mwendakulima wilayani Kahama, Julai 15, 2018. Kituo hicho kimejengwa kwa hisani ya mgodi wa Buzwagi wialayani Kahama.Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba, Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Stanslaus Nyongo na wapili kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa ACACIA, Asa Mwaipopo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la Majaliwa ambaye ni mmoja wa watoto waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Mwendakulima kilichopo Kahama baada ya kukizindua kituo hicho Julai 15, 2018. Kituo hicho kimejengwa kwa hisani ya mgodi wa Buzwagi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimbeba mmoja wa watoto waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Mwendakulima baada ya kukizindua kituo hicho kilichojengwa na Mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama Julai 15, 2018. Wapili kulia ni mama wa mtoto huyo aliyepewa jina la Majaliwa, Leticia Elias na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Social Plugin