MAGUFULI : WAKULIMA WANGEFANYA FUJO..NINGEANZA KIPIGO NA SHANGAZI WA WAZIRI MKUU

Rais John Pombe Magufuli amesema alikuwa akisubiri wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara wafanye fujo kama jinsi ambavyo Wabunge wa mikoa hiyo walivyokuwa wakidai na kueleza kwamba angewashughulikia kwa kipigo na angeanza na jimbo linaloongozwa na Waziri Mkuu.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake baada ya kuwaapisha Mawaziri na viongozi wengine ambao aliwateua siku ya jana alipofanya mabadiliko madogo katika wizara yake.

"Watu wanataka popularity, wengine nilisikia wanasema watachomewa nyumba, nilimwambia Waziri Mkuu nataka nione wakifanya fujo. Ningewapa kipigo. Tena ningeanza kwenye jimbo lake kama kuna shangazi zake ningeanza kupiga hao. Nasema ukweli wala sifichi"

Rais ameongeza "Lazima tufike mahali tuambizane ukweli, ndiyo maana nilimwambia Katibu Mkuu CCM, aende Dodoma siku ya kupiga kura. Wabunge wa CCM ambao hawakuwepo wachukuliwe hatua". 

Katika kuonyesha kukasirishwa na kitendo ambacho kilifanya na Wabunge wa Mikoa hiyo ambo pia ni wa CCM, Rais Magufuli amesema anashangaa wanafanya nini mpaka saizi kwenye Chama Cha Mapinduzi badala ya kuondoka.

"Watu wanashangilia uongo, tumechoka, nilimuuliza Waziri Mkuu kuna wabunge wangapi wa CCM, Mtwara na Lindi akasema wapo 17, nikasema bora waondoke wote, hata Waziri Mkuu ni wa huko naye angeondoka, bado tungeweza kuongoza nchi. Nilimpigia simu Katibu wa CCM tukae kwenye mpango huo. Wangeondoka,"

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema "Siku ya kupitisha bajeti nikamwambia Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru nenda Bungeni ukaangalie wabunge wangapi wa CCM hawapo bungeni uwalime barua, na kweli amewaandikia barua wote. Japo wapo Wabunge waliokuwa na sababu za Msingi lakini kuna wale ambao wamelimwa barua. Prof. Kabudi alikuwa amelazwa lakini kapokea barua yake na ataambatanisha na vyeti vya hospitali"

Mbali na hayo Rais amempongeza Naibu Waziri Mpya wa Kilimo na Umwagiliaji kwa kuweza kupambana kuitetea serikali wakati wa hoja ya Korosho ilipokuwa imepamba moto.

"Naibu Waziri wa Kilimo nakupongeza kwa kazi uliofanya Bungeni, huwa nafuatilia michango ya CCM, mwingine anasema tukienda hivi tutashindwa, kwa nini bado uko CCM, si utoke huko? Nakuomba ukashirikiane na wenzako Wizara ya Kilimo" amesema.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527