RAIS ATAKA RAIA WA KIGENI KULIPA KODI WANAPOFUNGA NDOA NA WANAWAKE WENYEJI


Mfalme Mswati wa Swaziland ametuma mswaada bungeni kuhusu kutungwa kwa sheria mpya kwa raia kutoka nje ya nchi hiyo kulipa kodi watakapofunga ndoa na wanawake nchini Swaziland kwa kutozwa kiasi cha 30,000 lilangeni ( dola 2,200) .


Mfalme Mswati ametuma mswaada huo bungeni huku akidai kuwa sheria hiyo ni kwa ajili ya kuwalinda wanawake nchini humo.

“ Lengo la sheria hii ni kuwalinda wanawake na matendo ya unyanyasaji kutoka kwa wapenzi wao wa kigeni wanaotumia njia ya kuoa wanawake wetu kwa ajili ya kupata uraia” amesema Msemaji wa Serikali Percy Simelane.

Aidha mswada huo umepingwa vikali na mmoja wa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake Dumsane Dlamini akidai kuwa sheria hiyo itawanyima haki wanawake nchini Swaziland maana wanawake hao huwapenda wanaume wa kigeni kwa utanashati na wanajua thamani ya mapenzi.

Lakini 2016, Wizara ya mambo ya Kigeni ilianzisha mpango wa kutoa uraia kwa wageni nusu milioni hasa kutoka Asia ambao watakuwa sehemu ya idadi ya raia 1.3 milioni ya wananchi wote wa Swaziland
Theme images by rion819. Powered by Blogger.