KOCHA KIM POULSEN AACHIA NGAZI


Aliyekuwa mshauri wa timu ya vijana nchini, Kocha Kim Poulsen.

Kocha Kim Poulsen ameamua kuachia ngazi timu ya vijana, ambapo alikuwa mshauri wa timu za vijana nchini kufuatia kukumbana na changamoto mbalimbali licha ya kufanya kazi hiyo kwa kipindi kirefu.

Kim ambaye amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu za taifa za vijana hapa nchini ajira ambayo alipewa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ameamua kuachia ngazi nafasi hiyo ambayo ameitumikia tangu mwaka 2016.

Kim Poulsen ambaye ni raia wa Denmark ameanza kazi hapa nchini akiwa kocha mkuu wa timu za vijana mwaka 2011 na kupandishwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars) mwezi Mei mwaka 2012 aliporithi mikoba ya Jan Poulsen.

Licha ya mkataba wa Kim kukatishwa mwaka 2014 ulipofika mwaka 2016 akawa mshauri wa ufundi kwa kushirikiana na aliyekuwa kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime na kuiwezesha Tanzania kucheza fainali za Afrika ikiwa ni kwa mara ya kwanza nchini Gabon mwaka 2017.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527