KIPIGO CHA YANGA KILIKUWA HAPA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 19, 2018

KIPIGO CHA YANGA KILIKUWA HAPA

  mtilah       Thursday, July 19, 2018

Yanga wamekubali kichapo cha mabao 4-0, katika kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Gor Mahia ya Kenya katika uwanja wa Kasarani jijini  Nairobi.

Mpaka kipindi cha kwanza kumalizika Yanga walikuwa nyuma kwa mabao mawili na walikuwa wamezidiwa takribani robo tatu ya mchezo.

Kipindi cha pili kinaanza Yanga walifanya mabadiliko kwa kutoka Yohana Mkomola na kuingia Said Mussa dakika 54, Mabadiliko mengine yalikuwa Ajibu alikwenda nje na kuingia Martine dakika 77 na alingia Tambwe akitoka Haji Mwinyi dakika 80.

Mabao ya mawili ya Gor Mahia kipindi cha pili yakifungwa na Haji Mwinyi aliyejifunga dakika 66 na pili ambalo lilikuwa la nne katika dakika ya 88 Ephrem Guikan ambaye alifunga mabao mawili katika mechi hii.

Ilikuwa hivi,  makosa ambayo Yanga waliyafanya katika kipindi cha kwanza hayo hayo yalijitokeza tena katika kipindi cha pili.

Makosa ya Yanga wachezaji wao hawakuwa fiti kulinganisha na wale wa Gor Mahia mabao walitoka katika mashindano ya Sport Pesa na Kagame Cup.

Kikosi cha Yanga hakikuwa kipana kwani hata katika kufanya mabadiliko yaani hawakuwa na mchezaji yoyote katika benchi ambaye angeweza kubadili matokeo au mchezo wenyewe.

Mabadiliko ya Yanga ambayo aliingia Tambwe, Mussa ka Martine hawakuweza kuisaidia timu hayakuweza kuisaidia timu kwani walikuwa wakizunguka na hata wakipata mipira walikiwa wakipoteza.

Mastraika wote wa Yanga katika mechi ya jana ni wazi walishindwa kufanya lolote kwani hata kikosi kizima kilishindwa kupiga shuti au shambulio lolote la hatari.

Mpaka mechi inamalizika Yanga walikuwa wameshikwa katika kila eneo kuanzia beki mpaka washambuliaji na walikuwa na kila sababu ya kufungwa.

Kama Yanga wanatoka kusonga mbele katika hatua ya makundi ingawa wananafasi finyu wanatakiwa kufanya mabadiliko ya kikosi kizima kwa kufanya usajili na kuongeza wachezaji wa maana.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post