KIGOMA YASHIKA NAFASI YA PILI KITAIFA KUWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

Mkoa wa Kigoma wapiga hatua Katika kuwezesha wananchi wake kiuchumi mkakati ulioanzishwa na serikali wa kuwainua wananchi kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla, umeonekana kuzaa matunda makubwa katika mkoa wa Kigoma kwa kuinua pato la uchumi kibiashara na shuguli za ujasiriamali kwa wanaume, wanawake na vijana.

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. Mstaafu Emanuel Maganga ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa kombe na cheti cha ushindi kwa nafasi ya pili kitaifa katika kuwezesha wananchi kiuchumi katika ukumbi wa utamaduni wilayani Kasulu.

 Maganga alisema juhudi kubwa ambazo zimefanywa na serikali ya mkoa wa Kigoma ni kusimamia na kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwa pamoja na kutoa mikopo, kuwapa elimu na mafunzo ya ujasiriamali wananchi kupita mabaraza ya biashara ya wilaya.

Afisa wa Dawati la Uwezeshaji Kiuchumi la mkoa wa Kigoma (RECO)  Deogratias Sangu ameeleza kuwa mafanikio ya kushika nafasi ya pili yametokana na kukidhi vigezo katika utekelezaji wa mambo yote yaliyopangwa kama msingi wa kuinua wananchi kiuchumi.

Sangu ameongeza kuwa Mwaka jana (2017) mkoa wa Kigoma ulishika nafasi ya tatu kitaifa, na kwamba juhudi kubwa imefanyika katika kuwezesha wananchi na kutekeleza vigezo vilivyowekwa kiushindani na kufanikiwa kufikia nafasi ya pili kwa mwaka 2018.

"Ninaamini ushindi huu umetupa hamasa kimkoa ya kufanya vizuri zaidi ili mwakani tuweze  kushika nafasi ya kwanza Kitaifa",alisema Sangu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na Malunde1 blog wawakilishi wa wananchi kutoka katika vikundi, Asasi na jumuiya za wafanyabiashara wameeleza kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na serikali ya mkoa  katika kuinua uchumi wa wananchi.

Serikali ya mkoa wa Kigoma imeahidi kuendelea kuwawezesha wananchi katika shughuli za ujasiriamali na uanziashaji wa viwanda vidogo ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa Mkoani humo, ili kutoa tija zaidi. katika biashar wanazofanya wajasiriamali hao.
Na Editha Karlo- Malunde1 blog Kigoma
Afisa wa dawati la uwezeshahi kiuchumi Mkoa wa Kigoma Deogratias Sangu akimkabidhi kombe la ushindi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga katika ukumbi wa utamaduni Wilayani Kasulu,kulia ni akishuhudia Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marko Gaguti. Picha zote na Editha Karlo- Malunde1 blog Kigoma
Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma(RAS) Amos Charles Pallangyo akionyesha kombe ambalo Mkoa wa Kigoma umeshinda baada ya kushika nafasi ya pili Kitaifa katika kuwezesha wananchi kiuchumi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527