
Kamanda Mwakyoma amesema kwamba ingawa taarifa za awali zinadai kwamba ni kufeli kwa breki ya nyuma, lakini zipo sababu za msingi ambazo zinaweza kutolewa na dereva huyo kwani tukio lililopelekea gari hilo kulipuka halikuwa la ghafla.
Akizungumzia ajali hiyo iliyotokea Tegeta usiku wa kuamkia jana, Kamanda Mwakyoma amesema kwamba basi hilo lilitokea Arusha likuwa na abiria 42, ambapo 22 walishukia Bagamoyo na wengine waliosalia walifikia maamuzi ya kushuka baada ya kuona gari linazidi kutoa harufu na ndipo dereva alipoamua kulitelekeza.
Aidha Mwakyoma ameongeza kwamba siyo kila ajali husababishwa na uzembe wa dereva kwani yapo mambo mengi ikiwepo nyaya za umeme kugusana, ku-jam kwa breki ya gari hivyo wamiliki wa magari wanapaswa kuwa makini wanapofanya 'service' ya magari ikiwa ni pamoja na kutazama mfumo mzima wa umeme na siyo kumwaga 'oil'.
Pamoja na hayo Mwakyoma amesema uchunguzi wa kina wa kuhusu ajali hiyo bado unaendelea kufanyika na sasa wanasubiria hati ya ukaguzi wa gari hilo kutokea Arusha kabla ya safari.
Social Plugin