DIAMOND PLATNUMZ AZUIWA KUFANYA SHOW NJE YA NCHI

BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa sababu msanii huyo hakuwa na kibali.


Diamond jana alikuwa akielekea katika visiwa vya Madagascar na Mayote ambako atatumbuiza leo (Julai 27) na kesho (Julai 28).


Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema Diamond alitakiwa kuondoka jana Saa 3.00 asubuhi lakini baada ya kuzuiliwa ilibidi aondoke saa 11.00 jioni baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali hicho.


“Ni kweli jana msanii wangu (Diamond) alikumbana na mkono wa Basata akiwa uwanja wa ndege. Kwa kuwa tulishalipwa hela ya watu ikabidi tukishughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini,” anasema.


Hata hivyo, alilaumu Basata kwa kushindwa kuweka wazi kanuni zake ili wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua.


“Ninashauri kama Basata wana chochote wanataka wasanii wakifanye wakishirikishe ili kuepusha mzozo,” anasema.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.