Wednesday, July 25, 2018

BABU WA MIAKA 71 AKUTWA NA NYARAKA BANDIA ZA SERIKALI .....VIMO VYETI 240 NA MIHURI 159

  Malunde       Wednesday, July 25, 2018
Na Dixon Busagaga ,Moshi
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka bandia za serikali 240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.

Nyaraka zilizo kamatwa ni pamoja na Vyeti vya kuzaliwa ,vyeti vya ndoa ,vyeti vya ubatizo,vyeti vya Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pamoja na mihuri mbalimbali miongoni mwao ikionyesha ni ile inayotumika wakati wa usajili vizazi na vifo katika manispaa ya Moshi na Kitete mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa alisema vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya kuandikia (Type Writer) na kifaa cha kuwekea namba huku akiwataja watuhumiwa kuwa ni pamoja na Athuman Selemani (71) anayetajwa kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa wilaya .


Wengine ni Justine Mziray (55) anayetajwa kuwa ni mtaalamu wa kuchonga mihuri,Sporah Daud anayetajwa kushiriki katika uandaaji wa nyaraka hizo kwa kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu (Type writer) na Costa Lyatuu anayetajw kuwa mtaalamu wa kughushi sahihi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mihuri iliyokutwa kwa mtuhumiwa huyo
Mihuri iliyokuwa ikitumika
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mashine aliyokuwa akitumia mtuhumiwa huyo kutengenezea nyaraka bandia za serikali
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post