BAADA YA MKWASA NA SANGA KUACHIA NGAZI, UONGOZI YANGA KUTOA TAMKO LEO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 24, 2018

BAADA YA MKWASA NA SANGA KUACHIA NGAZI, UONGOZI YANGA KUTOA TAMKO LEO

  Malunde       Tuesday, July 24, 2018
Baada ya viongozi wa Yanga kuzidi kuachia ngazi akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo jana, Clement Sanga kutangaza kujiuzulu wadhifa wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameitisha kikao na wanahabari leo.


Nyika ameitisha kikao hicho kuzungumzia mustakabali mzima wa Yanga juu ya kujaza nafasi za viongozi wake walioachia ngazi namna utakavyokuwa.


Ikumbukwe Yanga imekuwa haina Mwenyekiti kwa muda mrefu tangu kujiuzulu kwa Yusuf Manji akidai anahitaji kupumzika kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi binafsi.


Baada ya Manji, wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji akiwemo Salum Mkemi na Khalfan Hamis nao wameachia ngazi kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yao na uongozi wa juu wa klabu.


Kutokana na kujizulu kwao, uongozi wa Yanga kupitia kwa Nyika utaeleza kiunagaubaga leo hatma ya nafasi zao ikiwemo suala la uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyikiti pamoja na ile ya Katibu Mkuu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post