Wednesday, July 11, 2018

ASKARI POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI WIVU WA MAPENZI

  Malunde       Wednesday, July 11, 2018
KAMANDA wa Polisi Mkoani ya Mara Juma Ndaki amethibitisha kutokea kwa tukio la askari Polisi PC Nelson William G 3777 kujiua kwa kujipiga risasi kwa sababu za wivu wa mapenzi. 

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu leo jioni hii Kamanda Ndaki amesema askari huyo amejipiga risasi leo saa 8:30 mchana akiwa eneo la kambi za Polisi alikokuwa anaishi. 

Amefafanua kabla ya kujipiga risasi ameacha ujumbe kuwa ameamua kujua kutokana na wivu wa mapenzi kwa madai amekuwa hana mahusiano mazuri na mwanamke wake ambaye alikuwa ni mpenzi wake. 

Kamanda Ndaki amesema askari huyo kabla ya kuchukua uamuzi huo aliingia pia kwenye malumbano na mpenzi wake baada ya kwenda kwenye chumba cha mpenzi wake na kisha kuamua kuharibu mali alizonunua. 


Amesema baada ya tukio hilo la kuharibiwa mali mwanamke aliamua kwenda kutoa taarifa Polisi, kitendo ambacho askari William hakikumfurahisha kwani aliona kama amedhalilishwa. 

Hivyo akaona njia pekee ni kuchukua uamuzi wa kujiua na ilipofika muda huo akaamua kujiua kwa kujipiga risasi. 

Kamanda Ndaki alipoulizwa kama kuna mtu yoyote amekamatwa amejibu hakuna kwani askari ameacha ujumbe kuwa amejiua kwasababu hizo ambazo kimsingi ni wivu.

Amesema kwa sasa mwili wa askari huyo umehifadiwa chumba cha kuhifadhia maiti wakati taratibu za mazishi zikiendelea. 

Alipoulizwa kama askari huyo alikuwa wakiishi akiishi pamoja na mpenzi wake huyo,Kamanda Ndaki amejibu hawakuwa wakiishi pamoja kwani mwanamke alikuwa ana chumba chake na askari alikuwa anaishi kambini.
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post