MGANGA WA JADI MWENYE DAWA ZA KUZUIA RISASI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Mganga mmoja wa asili nchini Nigeria amefariki baada ya mteja wake kujaribu iwapo ana nguvu za kuzuia risasi kuingia mwilini mwake kama alivyodai.

Chinaka Adoezuwe , 26, aliuawa baada ya kumuagiza mteja wake kumpiga risasi alipokuwa akivaa nguvu hizo za kuzuia risasi katika shingo yake.

Maafisa wa polisi katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo wanasema kuwa mteja huyo sasa amekamatwa kwa madai ya mauaji

Nguvu za uganga ni maarufu nchini Nigeria , ambapo waganga huombwa kuwatibu raia magonjwa tofauti.

Lakini kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kula nguvu za kuzuia risasi na dawa.

Kijana mmoja alikuwa amemtembelea mganga huyo ili kupata nguvu za kuzuia risasi ambazo mganga huyo alimpatia, kulingana na mwanakijiji mmoja aliezungumza na gazeti la Punch.

Ili kuthibitisha kwamba nguvu hizo zinafanya kazi , alisimama na kumpatia mteja wake bunduki. Na hapo ndiposa janga likatokea!.

Mnamo mwezi Januari , muuzaji wa dawa za kienyeji alikamatwa baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kunywa maji ya kuzuia risasi kuuawa.

Muuzaji huyo anayeishi kaskazini magharibi mwa Nigeria aliripotiwa kumhakikishia mtu huyo kwamba hatofariki atakapopigwa risasi.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527