AJALI YA GARI YAUA DIWANI,DEREVA WA HALMASHAURI

Diwani wa Kata ya Mwanhuzi, Elias Shukia na dereva wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Haruna Ngata wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka koani Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka mara tatu.

Taarifa za awali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu zinaelea kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Mkiwa, Wilayani Singida.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumamosi Julai 14, 2018 Mtaturu amesema mkuregenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manuzi; mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Pius Machungwa na watu wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

Amesema majeruhi wanne wamelazwa katika hospitali ya St Gasper iliyopo Itigi na wawili wamelazwa hospitali ya Puma iliyopo wilayani Ikungi.

“Chanzo tulichokiona kwenye eneo la tukio ni kupasuka kwa tairi la mbele kushoto, hata hivyo tuwasubiri polisi wafanye uchunguzi zaidi watatuambia chanzo cha ajali yenyewe,”amesema.

“Ni gari ambalo lilibeba madiwani, mkurugenzi hajapata michubuko na tumemshauri apumzike kusubiri vipimo zaidi.”
Na Tumaini Msowoya, Mwananchi 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527