WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEA MZEE MAJUTO MUHIMBILI

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) jana tarehe 23 Juni, 2018 amemtembelea msanii nguli wa filamu Bw. Amri Athumani (Mzee Majuto) ambaye amefikia katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam akitokea India alipopelekwa na Serikali kwa ajili ya kupata matibabu.


"Serikali inafuatilia matibabu yako kwa ukaribu, hivyo usiwe na wasiwasi", alisisitiza Dkt. Mwakyembe akiongoea na Mzee Majuto. 

Akizungumza Mzee Majuto ameishukuru Serikali kwa kumhudimia na kumpeleka India kupata matibabu.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.