WANAWAKE WAKABANA KOO KANISANI WAKIGOMBEA KUKAA KARIBU NA MCHUNGAJI

Wanawake wawili nchini Kenya wamewashangaza wengi baada ya kuzozana na kukabana koo kanisani mbele ya Waumini wenzao wakigombania kukaa karibu na Mchungaji wa Kanisa hilo.

Inaelezwa kuwa mwanamke mmoja ambaye alifika kanisani akiwa amechelewa aligundua kuwa Mwanamke mwingine alikuwa ameketi katika kiti alichozoea kukaa ambacho kipo karibu na Mchungaji wa Kanisa lao.

Taarifa zinasema kuwa Mwanamke huyo alimwendea Mwanamke aliyekuwa amekaa karibu na Mchungaji na kumtaka anyanyuke ili akae kitu kilichoamsha mzozo na kuzaa ugomvi mbele ya Waumini wenzao.

Imeelezwa kuwa waumini ambao walibaki wanawashangaa ilibidi waingilie kati kuzima ugomvi huo huku wakidai kuwa waumini hao wanaliaibisha Kanisa lao.

Aidha kwa mujibu wa duru za kuaminika hazijaeleza kama Mchungaji huyo ana mahusiano na Wanawake hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527