Tuesday, June 19, 2018

MUME AUA MKEWE GESTI...NAYE AJIUA KWA KUJICHOMA KISU

  Malunde       Tuesday, June 19, 2018

Michael Daudi (31) Mkazi wa kijiji na Kata ya Bukokwa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, amemuua mke wake Tekla Lutandula (30) kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake kisha naye kujiua kwa kujichoma visu tumboni.


Tukio hilo limetokea leo alfajiri Juni 19 saa 11:00 asubuhi wakati wamelala nyumba ya wageni iitwayo 'Enjoy Guest House' katika Kijiji cha Kanyala Kata ya Bulyaheke wilayani Sengerema.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba chanzo chake ni wivu wa kimapenzi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bulyaheke, Musa Mwilomba alisema Tekla kwa sasa alikuwa akiishi katika Kijiji cha Kanyala na kwamba Daudi alimchoma Tekla visu 11 kisha na yeye kujichoma visu saba.

Mama mzazi wa Tekla, Devotha Shadrack amesema wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kifamilia na walishauriwa na kufikia muafaka na mwanaye alikuwa naye nyumbani kwao (kwa mama).

“Sikujua chochote kama mwanangu amelala gesti nimeshangaa kupata taarifa za mwanangu kuuawa,” amesema.

Mmoja wa wananchi waliokuwa wamelala ndani ya nyumba ya wageni aliyejitambulisha kwa jina moja la Magret alisema walisikia kelele lakini mwanaume huyo amedai atakayesogea atauawa.

Na Daniel Makaka, Mwananchi 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post