RAIS WA ZIMBABWE EMERSON MNANGAGWA ATUA BONGO


 Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa amewasili leo Alhamisi Juni 28, 2018 saa 5:30 asubuhi katika uwanja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Baada ya kuwasili amepigiwa mizinga 21, kukagua gwaride la heshima.

Mbali na Rais Magufuli, viongozi wengine waliofika kumpokea rais huyo wa Zimbabwe ni Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba; Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Baada ya mapokezi ya uwanjani, marais hao wameelekea Ikulu kwa mazungumzo zaidi.

Na  Elias Msuya, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.