UFARANSA,ARGENTINA,DENMARK NA CROATIA ZAFUZU 16 BORA KOMBE LA DUNIA


Croatia na Argentina zimefuzu kucheza hatua ya mtoano katika 16 za michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.


Argentina wamemaliza michezo yao kwenye kundi D wakiwa na alama 4 katika nafasi ya pili kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria jana usiku.


Mabao ya Argentina yaliwekwa kimiani na Lionel Messi mapema katika dakika ya 14 huku la pili likifungwa na Marcos Rojo mnamo dakika ya 86 ya kipindi cha pili.


Bao pekee la Nigeria liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Victor Moses katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili.


Wakati huo Ufaransa pamoja na Denmark zimefuzu kuingia mtoano baada ya sare ya kutofungana jana mchana katika mchezo wa kundi C.


Kutokana na matokeo hayo, Ufaransa sasa itakipiga dhidi ya Argentina katika hatua ya mtoano huku Denmark ikicheza dhidi ya Croatia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527