Tuesday, June 5, 2018

RAIS KUPOKEA KATIBA MPYA ALHAMIS

  Malunde       Tuesday, June 5, 2018
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuipokea Katiba mpya ambayo inaanza kutekelezwa siku ya Alhamis ambayo inatajwa kuwa itageuza mambo mengi kwenye taifa hilo, lakini pia kutoa fursa kwa Rais kuweza kuwania uongozi wa nchi hadi mwaka wa 2034.


Taarifa ya Ikulu ya Burundi imethibitisha kuwa sherehe za utiaji sahihi kwenye katiba mpya na kuitambulisha kwa raia zitafanyika katika mkoa wa kati wa Gitega eneo la Bugendana ambako huko ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa katiba.

Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi kuwa na sherehe za kuipokea katiba mpya,wataalam wa siasa za Burundi wanahisi utaratibu huo mpya ni ujumbe wa Rais Nkurunziza kukamilisha malengo yake ya kuitawala nchi hiyo bila kikomo.

Katiba pia inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukata kuketi meza moja na wapinzani.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post