MWENYEKITI WA KIJIJI ASHAMBULIWA KWA MISHALE NA MAPANGA


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati mkoani Manyara, Simon Lala ameshambuliwa na watu wasiojulikana waliomjeruhi kwa mishale na mapanga.


Tukio hilo limetokea leo Juni 18, 2018 katika kitongoji cha Waloa wakati mwenyekiti huyo kwa tiketi ya Chadema akiwa kazini pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema mwenyekiti huyo anahamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi baada ya kupewa rufaa na Hospital ya Mkoa wa Manyara.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Nicodemus Tarmo ambaye ni diwani wa Mamire kilipo kijiji hicho amesema chanzo cha tukio hilo lililotokea Juni 18, 2018 kati ya saa nne na saa tano asubuhi bado hakijajulikana.

Hata hivyo, Tarmo amesema taarifa zinadai tukio hilo linaweza kuwa limesababishwa na mgogoro wa ardhi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agostino Senga amesema hawana taarifa kuhusu tukio hilo.
Na Florah Temba na Joseph Lyimo, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527