MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MHADHIRI UDOM AKAMATWA

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limefanikiwa kumkamata John Mwaisango, mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Bi Rose Mdenye ambaye alifariki Dunia baada ya majeraha ya visu maeneo mbalimbali katika mwili wake.


Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo jana Juni18, 2018 kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Gilles Muroto, amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi na yupo mahabusu na kuongeza kuwa taratibu nyingine za sheria zitafuatwa ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

“Marehemu Rose Mdenye aliuawa kwa kukatwakatwa na visu na mtu ambaye inasemekana ni mume wake tunawajulisha kwamba huyu mtu tayari tumekwisha mkamata na anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, haya ni mafanikio makubwa” amesema Kamanda Muroto

Kamanda Muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alijificha katika Kata ya Mbingu, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambapo alikuwa amejificha baada ya kufanya tukio la mauaji ya mkewe.

Usiku wa Mei 25, 2018 katika eneo la Swaswa aliyekuwa mhadhiri wa masomo ya kompyuta katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Rose Mdenye, aliuawa baada ya kuchomwa visu mwilini na mtu ambaye anasidikiwa ni mume wake.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.