KWAYA YA UTUPU 'WANAFUNZI WAKIONESHA MAKALIO' YAZUA BALAA

Kanda ya video ya kwaya hiyo ilionekana wiki hii katika mashindano ya shule ikiwaonyesha wasichana waliokuwa wakicheza densi huku wakionyesha vifua vyao na makalio.

Densi ya 'utupu' ya kundi moja la kwaya ya shule nchini Afrika Kusini imevutia hisia za uchunguzi kufanywa kutoka kwa waziri wa elimu nchini humo.

Angie Motshekga alisema kuwa alisikitika baada ya kuona kanda ya video ya wasichana hao wa Xhosa wakicheza densi yao huku wakiwa wamevalia nguo inayojulikana kama "inkciyo".

Waziri huyo wa elimu ya msingi alisema kuwa ni ukosefu wa heshima kwenda kinyume na maadili ya tamaduni za taifa hilo.

Hatahivyo kiongozi wa kwaya hiyo ametetea hatua yao akisema kuwa ni fahari kubwa.

Kulingana na mtandao wa Daily Dispatch nchini humo, mwalimu huyo ambaye hakutajwa alisema: Ni fahari kubwa kucheza densi ya kitamaduni ya Xhosa. Tunafurahia 'inkciyo'. Ni fahari kubwa kwa wanawake na wasichana wa Xhosa.

Kabila la Xhsoa ndilo kabila la pili kwa ukubwa nchini Afrika Kusini.

Picha za densi hiyo katika mashindano huko Mthatha, mashariki mwa Cape ,zilionekana mapema wiki hii, zikiwaonyesha wasichana hao wakicheza densi huku vifua vyao na makalio yakiwa wazi.Waziri wa elimu ya msingi Angie Motshekga alisema kuwa mashindano hayo ni ya unyanyasaji

Kanda hiyo ya video ilipigwa wakati wa sehemu ya tamaduni ya Xhosa kulingana na mtandao wa Afrika Kusini wa Timeslive.

Swala hilo limewasilishwa katika idara ya kitaifa ya bi Motshekga.

"Ni makosa makubwa sana kwa baadhi ya walimu ambao wanafaa kujua zaidi ya kuwanyanyasa wasichana wadogo'' , chombo cha habari cha AFP kilimnukuu akisema katika taarifa.

"Hakuna makosa kupenda tamaduni na urathi wako , lakini hakukuwa na haja yoyote kucheza densi wakiwa utupu''.

"Tabia hiyo mbaya inaenda kinyume na maadili ya tamaduni zetu''.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527