HILI NDILO JENEZA LITAKALOBEBA MIILI YA MAREHEMU MARIA NA CONSOLATA

Hili ndilo sanduku/jeneza litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata likiwa tayari limekamilika kwa maziko hapo kesho  Jumatano Juni 6,2018 katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa

Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.

Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista waliokwishafariki.Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527