FAMILIA YAIOMBA SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WANAOZUSHA MZEE MAJUTO KAFARIKI

Baada ya kusambaa kwa taarifa katika kimtandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Muigizaji Mkongwe nchini, Mzee Amri Majuto, familia yake imeiomba serikali na vyombo husika ikiwemo mamlaka ya mawasiliano, kuwachukulia hatua watu wanaozusha taarifa za kifo kwa madai kuwa sasa ni mara ya 10.


Akikanusha taarifa za kifo cha muigizaji huyo kupitia kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na East Africa Radio, mtoto wa Mzee Majuto, Hamza Majuto amesema kuwa kama familia wameziona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na wala hawafahamu nia ya watu hao wanaozusha taarifa za kifo cha baba yake mara kwa mara.

Aidha mtoto huyo wa Mzee Majuto amesema kwamba baba yake kwa sasa anaendelea vizuri tangu aliporudi kutoka nje ya nchi na sasa (Majuto) yupo kwenye mapumziko kama jinsi ambayo inatakiwa.

"Tangu jana nimepokea simu na sms zaidi ya 500 zikitaka nithibitishe kuhusu kifo cha mzee. Kiukweli hii ni mara ya 10 kwa mzee kuzushiwa taarifa ya kifo. Natambua kwamba kuna vyombo vya usalama pamoja na mamlaka inayohusika na makosa ya mitandao hivyo hili la kuzusha kifo ni kosa la jinai naiomba basi TCRA ifuatilie ili kujua dhamira ya huyu mtu ambaye amekuwa akizusha taarifa za kifo" amesema Hamza.

Hata hivyo, Kijana huyo amesema kwamba kwa sasa wapo mapumzikoni lakini hawawezi kusema ni wapi kwa ajili ya kuepusha usumbufu ili kumsaidia mzee Majuto apate mapumziko mazuri.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527