DAKTARI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUIBA VIUNGO VYA MAREHEMU

Daktari mstaafu nchini Kenya Dkt. Moses Njue ameshtakiwa katika Mahakama ya Meru kwa kosa la kuiba viungo vya maiti za binadamu wakati wa utumishi wake.

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Claire Murithi ameiambia Mahakama kuwa Dkt. Njue aliiba moyo wa Polisi wa zamani wa nchi hiyo Benedict Karau huku akimtuhumu pia kupoteza ushahidi wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Mahakamani March 12, 2015 yalieleza kuwa Dkt. Njue ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa uchunguzi wa maiti katika hospitali ya Consolatha aliiba moyo wa Polisi huyo kabla haujapelekwa katika shule kwa ajili ya wanafunzi kufundishiwa.

Katika kesi hiyo ambayo imeendelea kusikilizwa , Dkt. Njue amekana mashtaka hayo huku mahakama ikimtaka kuweka dhamana ya zaidi ya shilingi milioni 45 za kitanzania.

Hata hivyo Wakili wa Dkt. Njue aliiomba Mahakama kupunguza dhamana hiyo kwa kile alichokidai kuwa mteja wake ni mtumishi wa umma ambapo baadae Mahakama ilimtaka kutoa zaidi ya milioni 11 za kitanzania kama dhamana.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.