BALOZI WA DENMARK ATUA KIGOMA KUKAGUA MIRADI YA UMOJA WA ULAYA

Balozi wa Denmark Einarl Jrnseni amewasili mkoani Kigoma akiwa ameambatana na mabalozi wenzake 10 kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kukagua na kuiendeleza miradi inayofadhiliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.

Akizungumzia ugeni huo mara baada ya kuanza kwa ziara ya Mabalozi hao leo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, iliyoanzia katika Mwalo wa Kibirizi uliojengwa kwa ufadhili wa nchi ya Denimark,Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga alisema  miongoni mwa miradi itakayotembelewa na mabalozi hao ni mwalo wa mazao ya uvuvi, Bandari ya Kigoma, meli ya MV Liemba na mradi mkubwa wa maji Manispaa ya Kigoma Ujiji uliofadhiliwa na Umoja huo kupitia Ubalozi wa Ujerumani.


Alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi wanayosaidia na kufadhili na kuendelea kutatua changamoto zingine zilizojitokeza huku akibainisha kuwa mradi ambao bado haujakamilika kati ya miradi hiyo ni mradi mkubwa wa maji ambao Mkandarasi wake ameshindwa kukamilisha pampu zinazochukua maji na kupeleka kwa wananchi baada ya zilizokuwepo kuharibika kutokana na mawimbi na baada ya mkandarasi kufirisika fedha za wafadhili zilihifadhiwa na serikali na ujenzi unaendelea ili kukamilisha mradi huo na aendelee kutoa ufadhili.

Akizungumzia mradi wa Mwalo wa Kibirizi Balozi wa Denmark Einarl Jrnseni alisema kupitia mradi wa Local Investment Climate unaofadhiliwa na serikali ya nchi hiyo imetoa kiasi cha shilingi milioni 677 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya mwalo huo na kuwasaidia wavuvi miundombinu ya kukausha mazao ya uvuvi pamoja na kujenga soko la kuuzia mazao hayo.


Alisema lengo la mradi huo ni kuongeza ubora katika kuboresha madhira ya biashara na kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya biashara na kuwasaidia wavuvi kufanya biashara yao kwa makini na kuwaongezea ubora wa mazao yao iliwaweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi kutokana na ubora wa mazao hayo.

"Tumekuja kuona Fedha zilizotolewa na Denmark kupitia Mradi wa LIC jinsi unavy endelea kuwasaidia wananchi na tumeridhika sana kwa kazi kubwa iliyofanyika katika mradi huu na tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Jumuiya ya Umoja wa Ulaya lengo ikiwa ni kuwasaidia wananchi kupata huduma sitahiki na kuinua uchumi wa wananchi wa maisha ya chini", alisema Balozi huyo.

Kwa upande wake Afisa uvuvi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Azizi Daudi alisema kutokana na mradi huo, mazao ya uvuvi mengi yamekuwa yakihifadhiwa baada ya vifaa vya kutengenezea barafu kukamilika na mwanzoni mazao hayo yalikuwa yakiharibika kutokana na joto lakini kwa sasa yanahifadhika.

Alisema hivi sasa mwalo huo una vifaa vya kuhifadhia samaki na vya kukaushia dagaa ambapo mpaka sasa wafanyabiashara na wengine wanasafirisha mazao hayo yakiwa na ubora na baadhi ya miundombinu ambayo bado haijakamilika wafadhili wameleta kiasi cha shilingi milioni 47 kwa ajili ya marekebisho ambapo mradi huo utaongeza uthamani kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog

ANGALIA PICHA
Mabalozi wa Umoja wa Ulaya wakikagua eneo la kuanikia Dagaa Katika Mwalo wa Kibirizi leo Manispaa ya Kigoma Ujiji Balozi wa Denmark nchini Tanzania Einarl Jrnseni (kushoto)








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527