ZITTO KABWE AUNGANA NA CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ametangaza nia ya kushirikiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Aikael Mbowe katika kupigania jimbo la Buyungu lililoachwa na Marehemu Mwalimu Kasuku Bilago.

Kupitia mtandao wake Zitto ameyaweka wazi hayo ambapo amesema kuwa kwa heshima ya Mwalimu Bilago yeye na Mbowe wamekubaliana kuwa watashawishi kuwepo na a Democratic Front Katika Jimbo la Buyungu. 

"ACT Wazalendo itaunga mkono mgombea wa CHADEMA au CHADEMA itaunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo. Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na Wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi" .

"Huu ni mwanzo wa harakati za kuwa na United Democratic Front dhidi ukandamizaji wa Demokrasia nchini na dhidi ya hali mbaya ya maisha ya watu wetu. Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha vyama vya Wafanyakazi, vyama vya wakulima, vyama vya wafanyabiashara na wananchi wengine," Zitto.

Uchaguzi wa Buyungu utafanyika baadaye mwaka huu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia Mei 26, 2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post