WAKAZI WA KANDA YA ZIWA WAENDELEA KUJIZOLEA ZAWADI ZA MZUKA WA SOKA NA COKA


Meneja Masoko na Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Nyanza, akiongea na waandishi wa habari.


Washindi mbalimbali wakikabidhiwa zawadi zao.
Baadhi ya washindi wakifurahia zawadi walizojishindia.
**
Promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka ya kampuni ya Coca-Cola Nyanza Bottlers ya jijini Mwanza inazidi kuwezesha wateja wa soda kujishindia zawadi ambapo wiki hii wateja 11 wamekabidhiwa pikipiki na wengine 4 wamekabidhiwa luninga bapa za kisasa.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,Meneja Masoko na Mauzo wa Nyanza Bottlers,Samwel Makenge ,alisema kumekuwa na ongezeko la washindi ,na kampuni inayo furaha kuona wateja wake wanaendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali.

“Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5,000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”,Alisema Makenge.

Washindi wapatao 15 ambao walikabidhiwa zawadi zao za Pikipiki naLuninga katika hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza, waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kiuchumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527