Utafiti : MALAZI YA SOKWEMTU NI MASAFI ZAIDI KULIKO YA BINADAMU

Malazi ya Sokwe mtu ni masafi kuliko ya binadamu, wanasayansi wamebaini. Viumbe hawa hujenga malazi kwa kutumia matawi na majani ya miti ambapo hulala.

Malazi ya sokwe mtu ni mfano kwa mwanadamu kijana ambaye anaweza kuona vigumu kufuata

Mwanafunzi wa Marekani wa shahada ya Uzamivu Megan Thoemmes, aliyeongoza jopo kukusanya sampuli za uchafu kutoka kwenye Sokwe watu 41 katika bonde la Issa nchini Tanzania: ''Tunajua kuwa makazi ya binaadamu yana aina mbalimbali ya viumbe.

''Mfano, takriban asilimia 35 ya vijidudu kwenye vitanda vya binaadamu vinatoka kwenye miili yetu wenyewe, ikiwemo, kinyesi, kinywani na vijidudu vya kwenye ngozi

''Tulitaka kujua ni kwa namna gani hali hii inaweza kufananishwa na Sokwe hawa,ambao huandaa vitanda vyao kila siku.

Ikilinganishwa na vitanda vya binaadamu, sehemu za kulala ya sokwe zilikuwa na aina mbalimbali za wadudu, matokeo ambayo hayakutarjiwa katika misitu ya kitropiki
Hata hivyo,uwezekano ni mdogo sana kwa sokwemtu kupata ''uchafu'' kinyesi, kinywa au bakteria kwenye ngozi.

''Hatukuona vijidudu kwenye malazi ya Sokwe mtu, jambo lililoshangaza kidogo'', alieleza Bi Thoemmes kutoka Chuo cha North Carolina .

Walishangazwa na walichokigundua walipojaribu kusafisha malazi ya hao chimpanzee kuondosha viroboto na chawa waliokuwepo.

Watafiti wanasema vitanda vya Sokwe watu ni visafi zaidi kuliko vya binadamu, ingawa viumbe hawa hutumia zaidi ya nusu siku kitandani.

Wanasayansi wamegundua kuwa malazi ya Sokwewatu nchini Tanzania yana kiasi kidogo cha kinyesi na bakteria kuliko magodoro ya binadamu majumbani, kwa sababu viumbe hawa huhama malazi kila usiku.
Chanzo- BBC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.