MWANASAYANSI ALIYESAFIRI KUFUATA KIFO KESHO NDIYO HATMA YAKE

Mwanasayansi aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall, kwa ajili ya kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu katika mshipa.


Kesho, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.


Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.


Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi.


Katika mahojiano Goodall amenukuliwa akisema "Natamani ningekuwa na uwezo wa kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka. 

"Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?


Goodall aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miaka 10 iliyopita baada ya kupoteza uoni na uwezo wa kutembea na alitamani kama kifo kingemchukua katika miaka hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527